VYAMA VYA USHIRIKA KAGERA KUCHUNGUZWA – MAJALIWA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atapeleka timu maalumu ya wataalamu mkoani Kagera watakaofuatilia na kuhakiki mali zote za vyama vya ushirika ili kujenga mfumo bora kwenye vyama hivyo kwa manufaa ya wakulima wa Mkoa huo. Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 20, 2021) wakati akizungumza na wananchi baada ya kuzindua jengo la Ofisi ya Mkuu wa